Loading...
 

Mashindano ya Hotuba za Ufahamu wa Jamii

 

Sustainability

 

Muda wa Hotuba

Mashindano ya Hotuba za Ufahamu wa Jamii yana lengo la kutafuta watu wenye uwezo wa kuhamasisha na kupata msaada wa kufanyia kazi matatizo ambayo dunia yetu inapatia.

Hotuba zinazoingia kwenye Mashindano ya Ufahamu wa Jamii hazitakiwi kuzidi muda wa dakika 7.

Mada ya hotuba lazima iwe tatizo ambalo watu wanalipitia, na jinsi ya kulifanyia kazi.

Hotuba kuhusu mada zingine au "matatizo" ya kubuni (kwa mfano., tunataka NASA kutuambia ukweli kuhusu uongo wa kutua kwenye mwezi) au yenye msingi wa sayansi ya uongo zitaondolewa.

Alama za Hotuba

Majaji watatoa alama za hotuba kulingana na vigezo vifuatavyo:

  • Usahihi wa kijamii (0 mpaka 10) - Watazingatia uhalisia na ukweli wa matatizo ambayo yameelezewa.
  • Utumiaji wa lugha (0 mpaka 10) - Watazingatia utajiri, maelezo, na uwazi wa lugha ambayo imetumiwa. Uwezo wa mzungumzaji kujenga picha kwenye akilli ya hadhira.
  • Utumiaji wa zana au visaidizi vya kuona (0 mpaka 10) - Watazingatia ufanisi wa visaidizi vya kuona au zana kwenye kukuza ujumbe wa hotuba.
  • Ubora wa masimulizi (0 mpaka 10) - Watazingatia utofauti wa sauti, lugha ya mwili, mapumziko, na sifa nyingine za usimulizi.
  • Uwepo wa hisia (0 mpaka 10) - Watazingatia uwezo wa msimulizi kufikisha na kuchochea hisia za wazi kwa hadhira.
  • Ujumbe wa Kijamii (0 mpaka 10)- Watazingatia kina cha ujumbe wa msingi wa hotuba. 
  • Ushawishi (0 mpaka 10) - Watazingatia ushawishi wa mzungumzaji na uwezo wake wa kuwafanya watu wafanye kitu.
  • Uwezekano wa kufanyiwa kazi (0 mpaka 10) - Watazingatia kama hotuba ilikuwa na mapendekezo ambayo yanaweza kufanyiwa kazi, uwezekano, na jinsi gani hadhira waliyapokea. 
  • Asili ya matendo (0 mpaka 10) - Wanazingatia uhalisia wa vitendo vilivyopendekezwa.

Kwa kila hotuba, wastani wa kila alama za hapo juu utatafutwa, na hiyo ndio itakuwa alama ya mwisho atakayopewa mshiriki.

KUMBUKA: Utumiaji wa zana au visaidizi vya kuona ni wa hiari. Kama mshiriki hakutumia zana au visaidizi vya kuona vyovyote, kipengele hiki kitatolewa kwenye kutafuta wastani wa alama.

Cheo

Mshindi wa ngazi yoyote isipokuwa Fainali za Dunia atakuwa na cheo cha "Mzungumzaji Bora wa Ufahamu wa Kijamii wa (kanda)"

 


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Saturday August 21, 2021 11:27:19 CEST by zahra.ak.